JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA

MUUMDO WA UPASHANAJI HABARI wa VINASABA VYA MIMEA

NINI MAANA YA MUUNDO WA UPASHANAJI HABARI WA VINASABA VYA MIMEA

Ni mtandao wa habari/taarifa kwa ajili ya kuboresha na kufuatilia uhifadhi na matumizi endelevu ya vinasaba vya mimea kwa ajili ya chakula na kilimo (PGRFA) Tanzania kwa kuzingatia utekelezaji wa Mpango wa Mkakati wa Dunia (GPA) juu ya Vinasaba vya Kilimo na Chakula (PGRFA).

Muundo huu ulianzishwa rasmi mwaka 2006 kutokana na michango washika dau nyeti wa kitaifa wanochangia katika uhifadhi wa vinasaba hivyo katika mazingira vinamopotikana, mashambani au mahali pengine na matumizi endelevu ya vinasaba hivyo, mali asili muhimu

DHifadhidata ya muundo huu inafanya kazi kama zana kuisaidia kamati ya kitaifa ya vinasaba vya mimiea na taasisi za Taifa katika kupanga mikakati na mipango Ya namna bora ya kusimamia vinasaba ya mimea


NINI MATUMIZI YA MUUNDO WA UPASHANAJI HABARI WA VINASABA VYA MIMEA

Muundo unatumika kwa uwazi ili:

fkuwezesha upatikanaji na tathmini ya taarifa za vinasaba vya mimea kwa ajili ya chakula na kilimo,
kuimarisha ushirikiano kati ya washika dau nyeti wa vinasaba vya chakula na kilimo (PGRFA)
kusaidia maamuzi, na
kuhifadhi kumbukumbu za kitaifa juu ya vinasaba vya kilimo na chakula (PGRFA).

Pia muundo huu unatoa nafasi kwa taaasisi zianzoshirika kuonyesha kile wanachofanya, kuchangia katika maamuzi na kupanua muonekano wao kitaifa na kimataifa.

Kutokana na taaarifa zilizomo kwenye muundo huu,  ripoti ya Tanzania  juu ya hali ya vinasaba vya mimea kwa ajili ya chakula na kilimo mwaka 2009 imeandaliwa. Imekwisha wakilishwa kwa kamisheni ya FAO juu ya vinasaba (PGRFA), kama change wa Tanzania katika kuandaa ripoti ya pili juu ya hali ya dunia kwa vinasaba vya mimea kwa ajili ya chakula na kilimo (PGRFA)

ZANA ZA MUUNDO WA UPASHANAJI HABARI WA VINASABA VYA MIMEA

Seti ya zana zilizokubalika na kamisheni ya FAO kwa ajili ya vinasaba vya chakula na kilimo:

Listi ya viashiria na mtindo wa ripoti, kutathmini utekelezaji wa Mpango mkakati wa dunia (Global Plan of Action); na
mfumo wa taarifa ikiwamo Hifadhidata na injini ya kutafutia, ambayo ina orodha fasaha ya taasisi za taifa zinazohusika na vinasaba (PGRFA), wataalamu, machapisho, sheria  na miradi, aidha aina za mazao


NAMNA UNAVYOFANYA KAZI

Kwa mchango wa hiari wa taasisi za kitaifa, unaosimamiwa na muwakilishi wa taifa wa GPA kwa kushirikiana na kamati ya kitaifa ya vinasaba vya mimiea.


NANI NA NAMNA YA KUSHIRIKI KATIKA MUUNDO WA UPASHANAJI HABARI WA VINASABA VYA MIMEA

Washikadau wote, hususani, taasisi za umma au binafsi, mashirika, kampuni ambazo zina mchango katika kuhifadhi na matumizi endelevu ya vinasaba vya mimea kwa ajili ya chakula na kilimo Tanzania inaweza kuwa sehemu ya muundo kwa kuwasiliana na.

Muwakilishi wa taifa wa GPA

Mr. Patrick Ngwediagi
Plant Protection Division, Ministry of Agriculture and Food Security
P.O. Box 9192
Dar es Salaam, Tanzania
Tel.: +255 22 2861404
E-mail:

au Muhifadhi wa muundo

Mr. Lourance Njopilai David Mapunda
National Plant Genetic Resources Center 
P.O. Box 3024,
Arusha, Tanzania
Email:

With the support from FAO
©Tanzania 2009